The House of Favourite Newspapers

Mohammed Dewji Adaiwa Kutaka Arudishiwe Mamilioni Aliyowapa Simba

0
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji.

Ikiwa ni siku mbili tu zimepita baada ya Simba kutiliana saini kandarasi ya udhamini na kampuni ya SportPesa, mdau wa klabu hiyo Mohammed Dewji ‘MO’ anadaiwa kuja juu na kutaka kurejeshewa fedha zake TZS 1.4 bilioni baada ya klabu hiyo kuvunja makubaliano waliyokuwa wameafikiana.

MO amesema kuwa anataka kulipwa fedha hizo ambazo alizitumia kuwalipa mishahara wachezaji wa Simba tangu mwaka jana.

Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov (kulia) akimkabidhi jezi mpya Rais wa Simba SC, Evans Aveva (katikati).

Uamuzi huu ameutoa baada ya klabu hiyo kuingia makubalino ya udhamini na kampuni ya SportPesa pasipo kumshirikisha yeye ikiwa ni kinyume na makubaliano.

Mei 12, 2017, uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, ulisaini kandarasi ya udhamini wa miaka mitano na Kampuni ya SportPesa yenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.

Katiba barua inayodaiwa kuandikwa na MO, amesema kuwa Simba wamekiuka makubaliano waliyokuwa wamefikia kwamba atoe fedha kwa makubaliano ya kuingia kwenye mfumo wa hisa, na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba, inabidi wakae meza moja viongozi na yeye na hiyo kampuni ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba. Lakini katika kandarasi ya SportPesa, MO amesema hakushirikishwa.
Simba tayari ilishaanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokuwa ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.

Leave A Reply