The House of Favourite Newspapers

Mo Dewji Ashinda Zabuni ya Kuinunua Klabu ya Simba

0
Mfanyabiashara bilionea kijana zaidi Afrika, Mohammed Dewjiameshinda zabuni ya kuinunua na kuiongoza klabu ya soka nchini, Simba Sc ambapo sasa klabu hiyo itawndeshwa katika mfumo wa kampuni.
Baada ya kushinda zabuni hiyo, ambapo atachukua hisa hadi 50 asilimia katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji aliingia ukumbini akiwa anasubiriwa kwa hamu na wanachama wa Simba.
Wanachama hao ndiyo waliopitisha uamuzi huo na kusubiri tume iliyokuwa inasimamia kupitia jaji mstaafu Mohayo kupitia mchakato na baadaye kutangaza.
Baada ya kutangazwa walishangilia kwa nguvu na baadaye Mo Dewji aliingia huku akishangiliwa kwa nguvu na baadaye akapewa nafasi ya kuzungumza na wanachama hao aliowashukuru na baadaye kuwaeleza nia yake na mipango yake ya uwekezaji.
Leave A Reply