The House of Favourite Newspapers

Mo Dewji Asimulia Alivyotekwa, Kufichwa na Kujikuta Chumbani – Video

IKIWA ni takribani siku 9 tangu kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji (MO) na hatimaye kupatikana usiku wa kuamkia leo baada ya kutelekezwa na watekaji hao katika maeneo ya Viwanja vya  Gymkana jijini Dar es Saalam, mfanyabiashara huyo amelieleza jeshi la Polisi namna ambavyo alitekwa.

Akizungumza na wanahabari nyumbani kwao na Mohammed Dewji, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema walipata taarifa za kupatikana kwa Mo Dewji majira ya saa 8 kuelekea saa 9 usiku, ambapo aliongozana na makachero wa polisi hadi nyumbani kwao na Mo kuthibitisha.

 

“Tulipata taarifa kwamba Mo amepatikana, na gari lile lile alilotekwa nalo ndilo limemchukua na kwenda kumuacha maeneo ya viwanja vya Gymkana, tumefika nyumbani na kuthibitisha kwamba amepatikana na anasema ana afya njema, hajapata maumivu makubwa, alikuwa kwenye mazingira magumu.

 

“Anachosema tangu apotee pale Colosseum alitembea kama dakika 15, kwa spidi kuelekea mahali ambapo alijikuta yupo kwenye chumba, lakini wakati wote huo walikuwa wameficha ili asiwaone watekaji.

 

“Lakini pia anasema waliomteka walikuwa wakiongea moja ya Lugha za Afrika Kusini, hivyo hofu yetu ni kwamba huenda walikuwa ni raia wa Afrika kusini, Jeshi la Polisi tunendelea na uchunguzi zaidi,” amesema Mambosasa.

 

Naye Mo dewji akazungumza.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama.” — Mohammed Dewji

Kipande cha video kinachothibitisha kupatikana kwa Mo Dewji alfajiri ya leo.

Comments are closed.