The House of Favourite Newspapers

Mo music: kama si ustaa ningeteseka!

0

mo musicStori: Boniphace Ngumije

MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amesema kuwa kama si ustaa angeteseka sana maishani kwani asingekuwa na koneksheni aliyonayo na wala asingekuwa na uwezo wa kuwafikia kwa urahisi wadau ambao kwa namna moja au nyingine wanampiga tafu.

Akipiga stori na safu hii, Mo Music alisema ustaa kwake umekuwa na msaada mkubwa ukizingatia elimu yake ni ya kidato cha nne.

“Unajua kuna kila sababu ya kuutumia ustaa watu vizuri maana kama tusingekuwa mastaa kuna vitu vingi tungevikosa, namshukuru Mungu nina jina lakini hainifanyi kubweteka na kulitumia kwa mambo mabaya,”  alimaliza Mo Music.

Leave A Reply