The House of Favourite Newspapers

Twanga Pepeta kutisha Miss Tabata, Julai 22

0

tabata2Stori: Burudani Mwanzo Mwisho

BENDI kongwe ya Muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta’ inatarajia kuangusha bonge la shoo katika shindano la kumsaka Miss Tabata 2016 litakayofanyika Julai 22, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Da West Park, Tabata jijini Dar.

Mratibu wa shindano hilo, Joseph Kapinga akizungumza na paparazi wetu alisema kuwa mbali na Twanga Pepeta kupagawisha siku hiyo, warembo 38 wanaendelea na mazoezi kujiandaa na shindano hilo linaloandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment.

Twanga (2)“Tunatarajia kufanya mchujo na kubaki na warembo 16 tu watakaopanda jukwaani siku hiyo ya Julai 22 wakisindikizwa na Bendi ya Twanga Pepeta chini ya Ali Chocky,” alisema Kapinga.

Naye mkurugenzi wa shindano hilo ambaye pia ni mkuu wa kambi, Godfrey Kalinga alisema warembo watakaoshiriki kwenye fainali watatembelea mbuga za wanyama ili kupromoti utalii wa ndani.

“Warembo watano watakaoshika nafasi za juu watashiriki kwenye shindano la Kanda ya Ilala yaani Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania,” alisema Kalinga.

Miss Tabata inadhaminiwa na Lete Raha, DataStar College, Global Publishers, CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti5 Kitwe General Traders na Bob Entertainment.

Leave A Reply