The House of Favourite Newspapers

MO SALAH, KLOPP KIMENUKA LIVERPOOL

Mohamed Salah ‘Mo Salah’

LIVERPOOL mambo yao ni mazuri kwa kuwa wapo kwenye mbio za ubingwa wa Premier League, lakini upande wa pili imeelezwa kuwa staa wa timu hiyo, Mohamed Salah ‘Mo Salah’ na kocha wake, Jurgen Klopp wameanza kutofautiana.

 

Wachambuzi wa masuala ya soka wanaeleza kuwa, Liverpool imekuwa na kiwango bora lakini kasoro ya wawili hao haizungumzwi kwa kiwango cha juu kwa kuwa mwendelezo wa timu ni mzuri.

 

Watu wa karibu wa mchezaji huyo wamesema kuwa ‘bifu’ yao imeenda mbali na imesababisha Mo aanze mpango wa kuomba kuondoka mwishoni mwa msimu huu. Habari hizo siyo nzuri kwa mashabiki wa Liverpool kipindi kama hiki lakini ndiyo ukweli unaoaminika kwa sasa.

 

Salah amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Liverpool kutokana na uwezo wake kuanzia msimu uliopita alipotua akitokea Roma. Wakala wa Salah aliulizwa juu ya taarifa hizo na vyombo vya habari vya Hispania, akakanusha lakini vyombo vingine vya Ufaransa navyo vikanukuliwa vikieleza kuhusu mchezaji huyo kutoiva na kocha wake.

 

Baada ya taarifa hizo, kumekuwa na maoni tofauti mengi kutoka kwenye mitandao ya kijamii huku mashabiki wengi wa Liverpool wakionekana kutofurahishwa na hicho kinachoendelea hasa wakati huu.

 

Vyombo vya habari vya England navyo vimejibu mashambulizi kwa kusema kuwa inawezekana hizo ni propaganda za vigogo wa Hispania kwa kuwa Liverpool itakutana na Barcelona wiki ijayo katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Salah amefunga mabao 23 na asisti 12 katika mechi 47 za msimu huu.

BREAKING: RAIS MAGUFULI AMWAGA MILIONI 5/MKIZILA NANYI MTALIWA

Comments are closed.