The House of Favourite Newspapers

Mobeto Awazima Wema, Uwoya

0

MWANAMITINDO grade one Bongo, Hamisa Mobeto anazidi kuwa wa moto balaa na kuendelea kuacha maswali kama yote juu ya; nini kilichopo katikati, kati yake na rapa Rick Ross wa Marekani?

 

Pili; Hamisa amewazima mastaa wenzake wa kike Bongo nzima kama Wema Sepetu, Irene Uwoya na wengine wote; yaani Hamisa ndiye anatrendi kuliko mastaa wote wa kike Bongo.

 

Ukiachana na masuala ya muziki na mitindo, Hamisa amekuwa na nguvu ya ushawishi aliyonayo ambayo ni kubwa mno ukimlinganisha na staa mwingine yeyote wa kike Bongo.

 

Kwa sasa Hamisa anatrendi na dili jipya la kinywaji kingine kutoka nchini Marekani ambacho balozi wake mkubwa ni rapa Lil Wayne baada ya kile cha mwanzo ambacho anaendelea na ubalozi wake ambacho balozi wake mkuu ni Rick Ross.

 

Baada ya Hamisa kuposti picha akiwa na kinywaji hicho kipya, Rick Ross amemjibu kwenye picha hiyo.

Hii inamaanisha kuwa, Lil Wayne na Rick Ross na marafiki zao wote wanamtambua Hamisa hivyo hahitaji sana kujitambulisha kwenye uwanja wa kimataifa.

 

Mbali na Rick Ross na Lil Wayne, pia msanii mkubwa wa Nigeria, Davido amekuwa akichati na Hamisa na wakati mwingine kuweka maoni kwenye posti za Hamisa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Mwigizaji na mtangazaji maarufu Bongo ameposti picha ya Hamisa na kuandika; “Waliokuwa wanaku-treat vibaya kuna siku watajutia kwa nini walikufanyia hivyo.

 

Kauli ya Mwijaku inatafsiriwa kuwa, kuna mafanikio makubwa zaidi yanazidi kumsogelea Hamisa.

Hayo ni madili machache tu ya kimataifa, lakini Hamisa ana madili mengi kuanzia ya nywele, vipodozi, nguo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mengine kibao.

STORI ZOTE; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply