The House of Favourite Newspapers

KISA MTOTO… MOBETO KUMBURUZA MZAZI MWENZIYE MAHAKAMANI!

0

Mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto, amemshitaki mzazi mwenziye ambaye ni Mbongo Fleva katika Mahakama ya Watoto, Kisutu jijini Dar, akidai kuombwa radhi na matunzo ya mtoto.

Wito huo kwa Mbongo Fleva, umewasilishwa na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.

Wakili Zulu alipozungumza leo, Alhamisi amesema mteja wao Hamisa Mobeto alimtumia Mzazi mwenziye notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.

“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,”.

Zulu amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.

Mobeto amezaa na jamaa huyo mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Prince Dully. Msanii huyo pia ni mzazi mwenza wa mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

NA ISRI MOHAMED/GPL

 

Leave A Reply