The House of Favourite Newspapers

Moi Alivyoitawala Kenya Miaka 24 kwa Mkono wa Chuma

0

MAPEMA wiki iliyopita rais wa pili wa Kenya, Daniel Arap Moi, ameaga dunia. Kifo chake kilitangazwa na Rais Uhuru Kenyatta, katika tangazo lililorushwa moja kwa moja na televisheni ya taifa.

 

Aidha, mtoto mkubwa wa Moi, Gideon Moi ambaye ni seneta, alisema baba yake amefariki kwa amani akiwa amezungukwa na familia yake hospitalini, saa 11.20 alfajiri Februari 4 mwaka huu. Gideon Moi pia ametoa shukrani za familia yake, kwa Wakenya wote waliomuombea marehemu baba yake.

 

UTAWALA WA MOI

Miaka 24 ya utawala wa Mzee Moi kutoka 1978 mpaka 2002, ilikuwa ni mchanganyiko wa maendeleo na utawala wa mkono wa chuma. Moi aliongoza Kenya kuanzia mwaka 1978 hadi 2002, utawala wake chini ya mfumo wa chama kimoja ukigubikwa na madai ya mienendo ya kiimla, uvunjifu wa haki za binadamu na ubadhirifu.

 

Licha ya shutuma hizo lakini, aliungwa mkono na Wakenya wengi kama nguzo ya umoja na utangamano katika taifa lake. Wanadiplomasia wanasema jaribio la mapinduzi dhidi yake miaka minne baada ya kuingia madarakani, lilishawishi siasa zake za kutawala kwa mkono wa chuma. Kabla ya kuwa rais, Daniel Arap Moi alikuwa makamu wa rais wa Kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.

 

Aliingia madarakani, mwaka 1978, baada ya kifo cha Jomo Kenyatta huu ulikuwa ushindi wake wa kwanza kisiasa baada ya kuwapika wandani wa Kenyata na hatimaye kukalia madaraka Mwanzo mwanzo wa utawala wake, Moi aliwataka Wakenya kuungana naye katika ujenzi wa Taifa, kwa kutumia kauli mbiu maarufu Nyayo, wakati huo nchi ilikuwa maarufu sana na nchi ilikuwa na maendeleo.

 

Lakini baada ya jaribio la mapinduzi ya mwaka 1982, Moi alibadilika sana na kuwa dikteta, aliyetumia nguvu kuzima uhuru wa raia, pamoja na wa kisiasa, kilichofuatia ni kuongezeka kwa ukabila, ukiukwaji wa haki za kibinadamu na mauaji ya kiholela. Neno Nyayo, lilibadilika sana badala ya kuwa neno la kuchochea uzalendo, likawa neno la kuogopwa.

 

Kumbukumbu ya nyumba za siri za mateso, ambapo raia wengi na waliodhaniwa kuwa maadui wa serikali walizuiliwa na kuteswa. Kufi kia mwaka 1990, Moi alikuwa kiongozi asiyetakikana mbali na kuwekewa vikwazo vya kimataifa, aliwekewa shinikizo kukubali vyama vingi vya kisiasa na kuweka ukomo muda wa urais.

 

Lakini badala yake, serikali ya rais mstaafu Moi, ilijibu hayo yote kwa polisi kuwashambulia viongozi wa upinzani, na wafuasi wao. Hatimaye Moi alisalimu amri, lakini kutokana na upinzani uliogawanyika, alishinda uchaguzi mara mbili mfululizo, mwaka 1992 na mwaka 1997.

 

Lakini msururu wa kashfa za ufi sadi zikiharibu kabisa sifa zake, mojawapo ya kashfa ilikuwa ile ya ‘Goldenberg’ iliyokuwa ya mabilioni ya dola ambayo ilihusu biashara ghushi ya kusafi risha nje dhahabu. Moi alihusishwa moja kwa moja na kashfa hiyo, japo yeye mwenyewe alikuwa akikanusha mara kwa mara kashfa hiyo. “Ni wendawazimu, anaweza kupeana mabilioni ya dola kwa kuambiwa kwa mdomo tu.

 

Muhula wake wa pili na wa mwisho, ulipomalizika mwaka 2002, Moi alimlazimisha Uhuru kumrithi. Lakini Uhuru Kenyatta ambaye alionekana kama kibaraka, alishindwa vibaya na muungano wa vyama vya upinzani ulioongozwa na Mwai Kibaki.

 

Wakati akistaafu na kumkabidhi madaraka Rais mpya, Moi alidhihakiwa na kufanyiwa mzaha na umati wa watu waliokuwapo kushuhudia akiondoka madarakani, lakini wachambuzi wanasema alikuwa na ushawishi wa kisiasa na aliishi na hatimaye kushuhudia.

 

Katika kifo chake, Wakenya watakumbuka jina la Daniel Toroitich Arap Moi, kwa upendo na heshima kubwa, lakini walioteseka chini ya utawala wake, watamsahau yeye na sifa zake haraka sana.

 

MOI NI NANI?

Moi alikuwa mmoja wa mwanasiasa wachache mashuhuri waliofanikiwa, ambaye hakutoka katika mojawapo ya makabila mawili makubwa nchini Kenya – Wajaluo na Wakikuyu. Alitoka jamii ndogo ya Tugen, mojawapo ya makundi yanayounganisha kabila kubwa la Wakalenjin.

 

Alianza kufanya kazi kama mwalimu mwaka wa 1945 katika shule ya African Government School na mwaka mmoja baadaye akiwa na umri wa miaka 22, akateuliwa kuwa mwalimu mkuu.

Kwa zaidi ya robo karne, Daniel arap Moi alitawala siasa za Kenya. Yeye alikuwa mwanasiasa aliyetaka kupendwa zaidi na wananchi kuliko alivyokuwa mtangulizi wake, rais wa kwanza wa jamuhuri ya Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

 

Hata hivyo, alishindwa kuvunjilia mbali utawala wa kiimla wa Jomo Kenyatta na badala yake yeye mwenyewe akajikuta katika hali ya kuwadhulumu wapinzani wake wa kisiasa.

 

Alibatizwa jina la “Profesa wa Siasa” kwa vile alivyoweza kukabiliana na wapinzani wake. Hata hivyo utawala wake ulimalizika na sifa mbaya kwa kuwa Serikali yake ilidumaza uchumi na ufi sadi ukashamiri.

 

Moi alizaliwa Septemba 2, mwaka 1924, katika jamii ya wakulima katika kaunti ya Baringo, katikati magharibi mwa Kenya. Jina lake la kwanza lilikuwa Toroiticha arap (mwana wa) Moi lakini baadaye akabatizwa katika Ukristo na kupewa jina la Daniel. Alipewa jina hilo la Wamishenari Wakristo akiwa mwanafunzi.

Leave A Reply