The House of Favourite Newspapers

Monalisa: Mwaka huu lazima nipige kura

0

Cdrisa4-1

Msanii wa filamu Bongo , Ivon Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’.

Mayasa Mariwata

ZIKIWA zimebaki siku tatu kuelekea uchaguzi mkuu, msanii mkongwe wa filamu Bongo , Ivon Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ amesema safari hii lazima apige kura, hata kama kutakuwa na foleni ya aina gani.

Akichezesha taya na paparazi wetu, Monalisa alisema bila kujali ustaa wake, siku ya uchaguzi atapanga foleni hata kama ni kubwa ili kutimiza azma yake ya kumpigia kura kiongozi anayefaa kuiongoza nchi.

“Japokuwa nina hofu, lakini lazima nikapige kura hivyo nawaomba Watanzania wawe watulivu na kudumisha amani, wakubaliane na matokeo ili kuepusha machafuko yasiyokuwa na maana ambayo yanaweza kuyagharimu maisha yetu,” alisema Monalisa.

Leave A Reply