The House of Favourite Newspapers

Mondi Aundiwa Mkakati wa Siri Kumuoa Tanasha

0

INAWEZEKANA watu wamechoka kumuuliza Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi swali la ataoa lini, ndiyo maana ameundiwa mkakati mzito wa kuhakikisha anamuoa mzazi mwenzake Tanasha Donna.

 

Chanzo kutoka ndani ya familia ya Mondi kililiambia Risasi Mchanganyiko hivi karibuni kuwa ndugu wa karibu na msanii huyo, wamekutana na kukubaliana kumuweka kiti moto Diamond.

 

“Hawataki mwaka huu uishe kabla Diamond hajafunga ndoa, na kwa kuwa kwa sasa yuko na Tanasha, wote wamekubali amuoe ili ajenge heshima,” chanzo kilisema na kuomba hifadhi ya jina.

 

KIGOGO ASIMAMIA MKAKATI

Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa mkakati wa kumbana Mondi kuoa unasimamiwa na kigogo mkubwa serikalini ambaye amekuwa hapendezwi na rukaruka ya Mondi kwa wanawake tofauti.

Ingawa chanzo hicho kilimtaja laivu kigogo huyo ambaye ni kijana, gazeti hili linahifadhi jina lake kwa sababu hakupatikana kuzungumzia jambo hilo.

 

Hata, hivyo baadhi ya viongozi wa dini akiwemo shehe wa mkoa wa Dar es Salaam; Alhad Mussa Salim, mara kadhaa wamekuwa wakimtolea mwito Diamond wa kuachana na maisha ya ukapera.

 

JINSI MONDI ATAKAVYOBANWA

Habari kutoka chanzo cha karibu na familia ya Mondi zimebainisha mkakati huo utakavyokuwa ambapo wazee wameandaliwa si kumshauri msanii huyo kufunga ndoa, bali kusimamia mchakato mzima.

“Uzuri ni kwamba Mondi hajachaguliwa mchumba, walichokubaliana wazee wa familia ni kusimamia hatua zote za kuelekea kwenye ndoa.

“Huyo kiongozi (kigogo) amesema yuko tayari wakati wowote kuwatuma wazee waende Kenya nyumbani kwao na Tanasha kukutana na wazazi wake na kutoa posa.”

 

Alisema kwa jinsi hali ilivyo zoezi hilo huwenda likafanyika hivi karibuni ambapo baba wa Mondi, Juma Abdul alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu mpango huo alihoji:

“Wewe unaonaje; Diamond akioa si ni heshima kwa familia, ungekuwa wewe kama mzazi ungekataa heshima ya mwanao?”

 

Naye dada wa Mondi, Esma Khan, alipoulizwa kuhusu hilo alijibu kama ambavyo Mzee Juma alivyojibu.

“Sisi tunasubiri maana hiyo naona itakuwa ni sapraizi, acha tuone, ndoa ni jambo la kheri,” alisema Esma.

 

NGONJERA ZA MONDI KUOA

Tangu akiwa na uhusiano wa kimapenzi na Miss Tanzania, 2006 Wema Sepetu, mara kadhaa alikuwa akitangaza kumuoa, jambo ambalo halikufanyika hadi uhusiano wao ulipoparaganyika.

Baada ya Wema, Mondi alijiweka kimapenzi kwa mrembo wa Uganda Zarinnah Hassan ‘Zari’ na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili ambapo pia aliahidi kumuoa lakini hakufanya hivyo na kuishia kumwaga.

 

Ngonjera mpya ya ndoa ya Mondi kwa sasa imehamia kwa Tanasha ambaye mara kadhaa amemuahidi kubariki uhusiano wao wa kimapenzi lakini ahadi haitimii jambo ambalo linatia hofu wadau kuwa huwenda yaliyomkuta Wema na Zari, yakamtokea Tanasha.

 

Leave A Reply