The House of Favourite Newspapers

Morrison: Huyu Wawa Ukiwa Naye Hukasiriki

0

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, raia wa Ghana, amefunguka kuwa amekuwa karibu na beki Muivory Coast, Pascal Wawa kutokana na kwamba akiwa naye hakasiriki.

 

Morrison ameongeza kwamba amekuwa na uswahiba na Wawa kutokana na damu zao kwenda sambamba kwa sababu ni mtu ambaye amekuwa akijichanganya kama ilivyo kwake.

 

Morrison ambaye ametua Simba akitokea Yanga, amesema kwamba anapenda kuwa karibu na Wawa kwa sababu ni mtu ambaye muda wote hamkasirishi.

“Ukaribu wangu na Wawa labda kwa sababu napenda sana kufurahia. Siku ya kwanza nilipojiunga niliona watu wachache ambao wanapenda kujichanganya kama mimi akiwemo Wawa.

 

Kuwa karibu na Wawa ni kama kiunganishi na yeye amegundua kuwa kuna kitu kinatuunganisha, hivyo damu zetu zimeiva.“Nimeona ukiwa naye wakati wowote huwezi kuchukizwa na jambo,” alimaliza Morrison.

STORI: SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave A Reply