The House of Favourite Newspapers

Moses Phiri; Jiwe walilolikataa waashi, anatupia tu Zambia

0

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Moses Phiri ambaye anakipiga kwa mkopo, Power Dynamos ya Zambia ameiokoa timu yake wakati ikiambulia pointi moja dhidi ya Zesco United.

Phiri aliisawazishia timu yake baada ya kutanguliwa kwa bao la dakika ya 34 lililofungwa na Collins Sikombe, ambalo lilidumu hadi zilipomalizika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Staa huyo amefunga bao hilo kwenye mchezo wake wa kwanza tangu ametua kikosini hapo akiisaidia timu yake kupata pointi moja na kupaa hadi nafasi ya tatu kwa pointi 37 ikiachwa pointi tano na vinara wa msimamo Red Arrows wenye pointi 42.

Phiri aliingia kwenye mchezo huo akitokea benchini na kuisawazishia timu yake katika dakika ya 87 na kuongeza idadi ya mabao ya kufunga kwa timu hiyo ambayo imecheza mechi 22 hadi sasa ikipachika jumla ya mabao 31.

Pawer Dynamos kwenye mechi 22 walizocheza wameshinda tisa, sare 10 na kufungwa michezo mitatu na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 17.

Leave A Reply