The House of Favourite Newspapers

Moto Wateketeza Matanki ya Mafuta ya Lake Oil Kigamboni – Video

0

Moto mkubwa umezuka usiku wa leo Jumatano Januari 8, 2020 katika hifadhi ya mafuta inayomilikiwa na kampuni ya Lake Oil iliyoko eneo la Vijibweni Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

 

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema wapo eneo la tukio katika jitihada za kuzima moto huo unaowaka kwa kasi.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri amesema kulikuwa na valvu ambayo ilikuwa inavuja mafuta na tayari imefungwa “Askari aliingia chini na akaifunga, moto umezimika”

 

RPC Temeke Amon Kakwale yupo eneo la tukio Kigamboni na amesema moto bado unawaka chini kwenye Chemba, haujashika matanki na Zimamoto wanaendelea na jitihada za kuuzima huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kuepusha watu kusogea na pengine kusababisha madhara.

 

Kamanda  Kakwale amesema moto bado unaendelea kuwaka na wanashirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuhakikisha hakuna madhara makubwa yatakayotokea.

 

“Sisi tupo hapa kama unavyojua wananchi wengi wanapenda kuona kwa macho matukio kama haya yakitokea kwahiyo tunasimamia usalama watu wasifike eneo la tukio,” amesema Kakwale.

 

Kakwale ameeleza wanafanya jitahada kuhakikisha malori mbalimbali ambayo hakutaja idadi yake kutokana na uwingi yanatolewa ndani ya eneo hilo ili kudhibiti maeneo yanayowaka moto.

 

“Hakuna taarifa zaidi ya madhara ukiacha kuungua kwa matanki ila kwakuwa tupo hapa tutaendelea kutoa taarifa zaidi,” amesema Kakwale.

 

Leave A Reply