The House of Favourite Newspapers

Moto Wateketeza Nyumba 19 Rufiji – Video

0

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge pamoja na wajumbe wa kamati ya usalama ya wilaya ya Rufiji wamefika kwenye tukio la moto lililotokea usiku wa kuamkia leo ili kuona athari iliyotokea na jitihada ambazo uongozi wa wilaya wamezichukua kuhakikisha wananchi wanakuwa salama katika kitongoji cha Shaurimoyo kijiji cha Nyamwage Kata ya Mbwara ambapo nyumba zaidi 19 zimeteketea kwa moto.

 

Inadaiwa kuwa tukio hilo limetokea baada ya mwananchi mmoja akiwa anasafisha eneo lake moto ulimshinda na kuteketeza nyumba zipatazo 19 za wananchi pamoja na mali na thamani zilizopo ndani ya nyumba hizo na hakuna majeruhi yoyote katika ajali hiyo.

Aidha Abubakari Kunenge ametoa pole kwa serikali ya wilaya pamoja na wananchi waliokutwa na madhara hayo na kuwapongeza wakazi wa maeneo ya karibu kuweza kuwapatia hifadhi wananchi wenzao waliokutwa na ajali hiyo na kuwaagiza uongozi wa wilaya hiyo kufanya haraka kujua tathmini ya athari iliyopatikana ili kuweza kuwasaidia waliopata ajali hiyo.

 

Kwa upande wake Mkuu wa wailaya ya Rufiji Meja Edward Gowele ameeleza kama wilaya hatua walizochukua mara baada ya kutokea tukio hilo na kutoa rai kwa wakazi wa wilaya hiyo kuwa makini wakati wanachoma moto kwani kwa sasa ni kipindi cha upepo mkali.

 

Wananchi wa eneo hilo nao wameeleza tukio jinsi lilivyowaathiri hivyo kuomba serikali kuweza kuwasaidia kwa haraka maana hawana mahala pakuishi.

Leave A Reply