The House of Favourite Newspapers

Mr Shinda Nyumba Aitikisa Kigamboni

Wadau wa Mji Mwema-Kigamboni jijini Dar wakiwa kwenye pozi na mabango ya Shinda Nyumba.

Mr Shinda Nyumba akiwa kwenye pozi na wasomaji wa Kigamboni.

Mr Championi akiwa kwenye pozi na wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers.

Mr Shinda Nyumba akitoa maelekezo kwa wasomaji wa Kigamboni. 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Jimmy Haroub akitoa maelekezo kwa wasomaji wa Kigamboni.

Wasomaji wa eneo la Tungi-Kigamboni, Pendo (kushoto) na Sikuzani wakielekezana namna ya kujaza kuponi.

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Keffa Masaga akitoa maelekezo kwa wakazi wa Mwembemtengu-Kigamboni, jijini Dar.

Jimmy akiwa na wasomaji wa Kigamboni.

Mr Championi akiwa na wasomaji kwenye picha.

Wasomaji wa Tuangoma- Kigamboni, Masoud na Mohamedi akiwa kwenye pozi na magazeti yao.

Mr Shinda Nyumba akiwa kwenye picha ya pamoja na wananchi  wa Kigamboni.

STORI: Na Gabriel Ng’osha | GPL

WAKAZI na wasomaji wa Magazeti Pendwa ya Kampuni ya Global Publishers, leo wamejitokeza kwa wingi katika kumkabidhi kuponi za Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, Julius Charles ‘Mr Shinda Nyumba’ ambaye amekuwa akizunguka katika viunga mbalimbali vya Jiji la Dar.

Mr Shinda Nyumba ambaye aliambatana na Mr Championi walipotoa zawadi ndogondogo kwa wakazi wa maeneo ya Tuangoma, Mwembemtengu, Mikwambe, Kibada, Mji Mwema na Tungi katika Jimbo la Kigamboni, jijini Dar.

Katika promosheni hiyo, Mr Shinda Nyumba alikuwa kivutio kikubwa kwa wasomaji ambapo alipokelewa kwa shangwe kila alipopita.

Mr Shinda Nyumba amewahimiza wasomaji kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano hilo ili kuingia moja kwa moja katika droo ndogo ya kwanza itakayochezeshwa Februari 8, mwaka huu kwenye Viwanja vya Zakhem-Mbagala jijini Dar.

“Niwaombe wasomaji mjitokeze kwa wingi katika droo ya kwanza, kwani nitagawa zawadi mbalimbali nyingi, na pia endeleeni kununua Magazeti ya Global na kujaza kuponi ili kujiongezea nafasi ya kuwa washindi wa zawadi mbalimbali kabla ya ile kubwa ya Nyumba,’’ alisema Mr Shinda Nyumba.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Comments are closed.