The House of Favourite Newspapers

Msafara wa Makonda Wapata ajali Masasi ukitokea Ruvuma

0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Paul Makonda.

Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Paul Makonda umepata ajali mchana wa leo, kilometa chache kabla ya kufika Masasi ukitokea Ruvuma baada ya magari takribani tisa kugongana.

Mapema leo, Makonda alitangaza kusitisha ziara yake mkoani Ruvumakufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ambnapo msafara wake uliianza safari kuelekea jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka eneo la tukio, zinaeleza kwamba watu saba wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Masasi huku Makonda akiwa salama kwani gari alilokuwa amepanda, halikuhusika kwenye ajali.

Leave A Reply