MSAIDIZI WA MEMBE ALIYEDAIWA KUTEKWA APATIKANA

MSAIDIZI wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, Allan Kiluvya amepatikana akiwa hai baada ya kuachwa na wanaodaiwa ni watekaji wake katika eneo la Njia Panda ya Segerea jijini Dar es Salaam leo na baada ya kupatikana ameongea na wanahabari kutoka shukurani zake.

 

Akizungumza kwa namna alivyoachiwa Kiluvya amesema; “Nilishushwa sehemu ambayo niliona ni sehemu salama kwa sababu nilieweza kupata usafiri wa kurudi kwangu.”

 

“Wao wenyewe (Wanaodaiwa kuwa Watekaji) waliniuliza ni wapi tukikushusha unaweza kufika salama? Nikawauliza kwani tupo wapi? Wakasema tupo Gongo la Mboto. Nikasema mimi nakaa Kinyerezi mkinishusha njia panda ya Segerea nitakuwa salama.”

 

Aidha, kwa sababu suala hilo lipo Polisi amesema kuwa hawezi kuelezea ni nini kilitokea huko alikokuwa bali tusubiri tamko au ripoti ya Polisi. “Kwa kuwa mimi ni Mkweli sana na najua Polisi watasema kile nilichosema.”

 

Lakini pia alipohojiwa kama ataendela kuwa Msaidizi wa Membe, Allan amesema kuwa anatumaini ataendelea kuwa Msaidizi wa Waziri huyo wa zamani kwani amekuwa msaidizi wake tangu mwaka 2012 akiwa Mwanafunzi wa Chuo hadi sasa

 

Awali, alianza kutoa shukurani zake kwa Wanahabari kwa namna ya walivyojitolea kuhakikisha sauti za familia yake, Wanasiasa na Watanzania wote zinasikika. Pia amemshukuru Membe, IGP Sirro na Polisi wote wa Kituo cha Kawe.

MAJERUHI WA AZAM HOI KITANDANI AZUNGUMZA – VIDEO


Loading...

Toa comment