The House of Favourite Newspapers

Msanii wa Bongo Movie Gift Azikwa Makaburi ya Kinondoni

mazishi-ya-msanii-gift-16
Jeneza lenye mwili wa marehemu Gift.
mazishi-ya-msanii-gift-1
Shamsa Ford (kushoto) na Johari wakilia kwa uchungu baada ya kutoa heshima zao za mwisho.
mazishi-ya-msanii-gift-2
Msanii wa maigizo Johari akipita mbele ya jeneza kutoa heshma za mwisho.
mazishi-ya-msanii-gift-3
Msanii Shamsa Ford akipita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho.
mazishi-ya-msanii-gift-4
Jacob Steven ‘JB’ akipita mbele ya jeneza kutoa heshima zake za mwisho.
mazishi-ya-msanii-gift-5
Mkongwe wa maigizo hapa nchini, Mzee Chilo akisaidiana na waombolezaji kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu Gift.
mazishi-ya-msanii-gift-6
Mume wa marehemu, John Lister (kulia) akilia kwa uchungu.
mazishi-ya-msanii-gift-7
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili.

mazishi-ya-msanii-gift-8 mazishi-ya-msanii-gift-9 mazishi-ya-msanii-gift-10 mazishi-ya-msanii-gift-11 mazishi-ya-msanii-gift-12 mazishi-ya-msanii-gift-13 mazishi-ya-msanii-gift-14 mazishi-ya-msanii-gift-15

Hatimaye mwili wa aliyekuwa msanii wa Bongo Movie, Gift John aliyefariki juzi katika Hospitali ya Sinza- Palestina baada ya kuugua, umezikwa leo katika Makaburi ya Kinondoni.

Kabla ya mazishi, wasanii mbalimbali wa Bongo Movie walipata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu, shughuli iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Njiapanda ya Segerea, Dar ambapo wasanii wengi wa tasnia ya filamu Bongo walihudhuria.

Marehemu Gift, pia alikuwa ni mke wa muongozaji maarufu wa filamu, John Lister. baada ya ibada fupi iliyofanyika nyumbani marehemu, mwili wa Gift ulipelekwa Makaburi ya Kinondoni ulikopumzishwa.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina!

Na Denis Mtima/ GPL

Comments are closed.