The House of Favourite Newspapers

Msanii wa Chuz Apandisha Mashetani

0
Tuesday Kihangala ‘Chuz’.

 MAYASA MARIWATA, GAZETI LA AMANI, HABARI

MWIGIZAJI aliye chini ya mkongwe wa filamu za Kibongo, Tuesday Kihangala ‘Chuz’, Angel Jackson ‘Kibibi’ anadaiwa kupandisha mashetani akiwa kwenye kambi ya kurekodi tamthiliya mpya huko Lushoto jijini Tanga akidai kuwa wenzake wanamuibia nyota yake.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kambini humo, tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita ambapo Angel alikurupuka na kuanza kupiga mayowe na kujigaragaza huku na kule akidai wenzake wanamchezea usiku kwa lengo la kuchukua nyota yake.

Chanzo hicho kilifunguka kuwa, wakati Angel akikutwa na mkasa huo, wenzake nao walimshutumu kuwa yeye ndiye huwa anawafanyia mambo ya ajabu kuvuta nyota zao hivyo mambo hayo ya maruweruwe yalikuwa yamemrudi. Kufuatia sekeseke hilo, paparazi wetu alimvutia waya Chuz juu ya ishu hiyo ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Siwezi kulizungumzia tukio hilo, kwani wakati linatokea sikulishuhudia.

Leave A Reply