The House of Favourite Newspapers

Msanii wa Muziki wa Injili, Gladness Mwanga Aachia Ngoma Mpya, Kaa Nami

0

 

Miongoni mwa Wasanii chipukizi wa Injili wanaofanya vizuri kwa sasa ni pamoja na Gladness Mwanga ambaye anatamba na kibao chake cha ‘Kaa Nami’ Alichokiachia siku chache zilizopita na kupokelewa vizuri na Wadau wa Injili Nchini.

 

Ukisikiliza kibao hicho unaweza usiamini kwamba ndio wimbo wake wa kwanza kuuachia Rasmi baada ya kufanya ‘Cover’ za wasanii wengine kwa muda mrefu.

 

Cristina Shusho na Martha Mwaipaja ndio watu walimshawishi zaidi Gladness kuingia kwenye muziki kwani Kila alipokuwa akiwasikiliza alikuwa akifurahi na kutamani kufanya kama wao.

 

Ukimuuliza Gladness Sababu za kuingia kwenye muziki atakujibu tofauti kabisa kwani wasanii wengi wanafanya muziki kama Sehemu ya biashara ila kwa upende wake Lengo kuu la kuimba ni kutangaza Injili.

 

Leave A Reply