The House of Favourite Newspapers

Mshambuliaji Mpya Yanga SC Kutua Wiki Ijayo

0

UONGOZI wa timu ya Yanga umesema kuwa unatarajiwa kumpokea mshambuliaji wao mpya Sadio Ntibazonkiza mara baada ya kumalizika kwa mapumziko mechi za timu za taifa zinaoendelea kufanyika duniani kote.

 

Ntibazonkiza mwenye uraia wa Burundi alisajiliwa na Yanga Oktoba 12 akiwa na timu ya taifa ya Burundi ilipokuja kucheza na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambapo mchezaji huyo aliifungia timu yake bao pekee ambapo Burundi walishinda kwa bao 1-0.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Afisa Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, alisema kuwa kiungo huyo kwa sasa yupo katika majukumu ya timu ya taifa ya Burundi na mara baada ya kumalizika michezo hiyo atakuja kujiunga na rasmi na Yanga tayari kwa kuanza kucheza.

 

“Ntibazonkiza kama ambavyo tuliwataarifu awali kuwa atarejea nchini mara baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili, kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Burundi hivyo baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa atakuja rasmi kujiunga na kambi ya Yanga.

 

“Ujio wa Ntibazonkiza ni ongezeko la mchezaji mwenye uzoefu kwenye kikosi chetu jambo ambalo naamini litatusaidia kuhakikisha tunazidi kufanya vizuri kwenye michezo yetu ya ligi,”alisema kiongozi huyo. Burundi wanatarajia kucheza na Maurtania leo na watarudia Novemba 15 na hivyo Novemba 16 staa huyo ataanza safari ya kutua nchini.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave A Reply