The House of Favourite Newspapers

Mshambuliaji wa Yanga Aziz Ki Aahidi Kuwaua Waarabu kesho nchini Tunisia

0
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mburkinabe, Stephane Aziz Ki.

 

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mburkinabe, Stephane Aziz Ki, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia ni lazima washinde mchezo wa kesho Jumatano dhidi ya Club Africain ya nchini Tunisia.

 

Timu hizo zitavaana katika mchezo wa marudiano wa Play-Off wa Kombe la Shirikisho Africa baada ya ule wa awali uliopigwa Dar, kutoka suluhu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Aziz Ki alisema yupo tayari kuipambania timu hiyo na kuipa matokeo mazuri ya ushindi.

 

Aziz Ki alisema kwa kushirikiana na wenzake, atapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo.

 

Aliongeza kuwa, anafahamu machungu waliyoyapata mashabiki wao katika mchezo wa kwanza waliocheza Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

“Tunafahamu tuna kibarua kigumu cha kuipa timu yetu matokeo mazuri, hivyo ni lazima tupambane ndani ya uwanja.

 

“Hatutakubali kupoteza mchezo huu, kwani tunafahanu umuhimu wake ambao ni lazima tupate matokeo mazuri.

 

“Hivyo kwangu nitahakikisha ninatimiza majukumu yangu uwanjani ili tupate matokeo mazuri.

 

“Ninaahidi kutumia vema kila nafasi nitakayoipata kuhakikisha nafunga,” alisema Aziz Ki.

STORI: WILBERT MOLANDI

MWILI wa RUBANI MSAIDIZI ALIYEFARIKI KWENYE AJALI ya NDEGE BUKOBA WAAGWA, VILIO VYATAWALA..

Leave A Reply