The House of Favourite Newspapers

Msichana wa Miaka 9 Anusurika Kifo Baada ya Kumpiga Mamba Kwenye Pua Yake

0

Mtoto mwenye umri wa miaka tisa amenusurika kifo kutokana na shambulio la mamba katika wilaya ya Chibuto katika jimbo la Gaza, kusini mwa Msumbiji.

Msichana huyo alikuwa akiogelea katika mto Limpopo wakati kisa hicho kilipotokea.

Aliviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba alipogundua kuwa alikuwa ameshambuliwa, alijaribu kukwaruza pua ya mnyama huyo ambaye, kabla ya kumwachia, alimsababishia majeraha mabaya kwenye mguu wake mmoja.

“Mamba alinishika na kuniburuta nami nikampiga na kukwaruza pua yake.

Ghafla mamba aliniachia mara moja na kunitupa,” alimwambia mtangazaji wa Radio ya serikali ya Msumbiji.

Alipelekwa katika hospitali ya eneo hilo kwa matibabu. Marta Moiane, mkurugenzi katika hospitali hiyo, amesema msichana huyo yuko katika afya njema.

Dkt Moiane alisema hii ni mara ya pili katika mwaka huu kwa hospitali hiyo kulaza mtu kutokana na shambulio la mamba.

Mashambulizi ya mamba ni ya kawaida katika mito mikuu ya Msumbiji na vijito vyake.

MANZOKI na LUIS MIQUISSONE WATUA SIMBA, YANGA YAPATA DILI SUDAN | SPORT ZONE

Leave A Reply