The House of Favourite Newspapers

Msisherekee Tambwe Kulipwa, Angalieni Msingi Wa Tatizo, Mjiulize…

0

UMEWASIKIA Yanga, wamesema watalilipa lile deni wanalodaiwa na mshambuliaji wao wa zamani, Amissi Tambwe raia wa Burundi.

Wanatakiwa kulipa zaidi ya Sh milioni 44 kutokana na fedha za usajili pamoja na zile za mishahara za Mrundi huyo ambazo zilicheleweshwa bila ya sababu.

 

Kama sababu zilikuwepo, pia huenda hazikuwa na nguvu ya kuzuiwa kulipwa kwa deni hilo la Tambwe kwa kuwa kungekuwa na mpangilio hata wa kulipunguza taratibu.

 

Ingewezekana makubaliano kati yao na Tambwe yangewasaidia sana na mwisho hili lingeisha Yanga wakilipwa fedha wanayodaiwa tu. Lakini sasa kutokana na tishio la kufungiwa miaka mitatu kufanya usajili, Yanga wataingia katika presha na mambo mawili yatawatokea.

 

Kwanza ni kutoa fedha katika sehemu ambazo zilikuwa zina bajeti nyingine na kulipa kwa mara moja, fedha ambazo wangeweza kulipa taratibu, moja baada ya nyingine huku wakiendelea na mambo yao.

 

Sasa ni zote kwa wakati mmoja na hakuna mjadala. Maana yake kuna vitu watalazimika kuvuruga kwa asilimia kubwa ili kulipa hilo deni.

 

Hawana ujanja kwamba hawatavuruga kwa kuwa kama walishindwa kulipa kwa wakati mmoja hapo awali, hata sasa hawana nguvu hiyo zaidi ya kujitutumua.Pili, Yanga wataingia hasara. Wanakwenda kulipa fedha zaidi ya waliyokuwa wanadaiwa na Tambwe.

 

Najua hili hawataki kwenda kuwaambia wanachama na mashabiki wao na badala yake jambo hili linataka kupelekwa kisiasa, si sahihi.Yanga italipa zaidi kwa kuwa kuna gharama za uendeshaji kesi, hizi pia zitahusu gharama za wakili wa Tambwe. Maana yake kama wangelipa deni mapema na kwa maelewano na Tambwe na ingewezekana kidogokidogo, wasingeingia katika hasara hii.Nimeona sehemu kadhaa katika mijadala mingi suala hili linachukuliwa kama utani wa mashabiki au baadhi yao kutaka kuonyesha Yanga haina shida italipa mara moja.

 

Kulipa mara moja, ndio. Lakini jiulize, kwa nini hiyo mara moja isifanyike kabla ya hapo na ujue wakati fulani Yanga walikata rufaa na kulipa mamilioni ya fedha, wakashindwa kumalizia gharama ya rufaa.

 

Ulivyo utaratibu wa Fifa na Cas, unarudishiwa fedha yako lakini kiasi SALEH ALLY,Dar es Salaamkinakatwa, hiyo ni hasara. Maana yake, hii ilikuwa ni kengele tosha ya kuonyesha kwamba kesi hiyo baadaye inaweza kuja kuwa tatizo kwa Yanga.Kufurahia Yanga inakwenda kutoa zaidi ya Sh milioni 44 kwa mchezaji ambaye hajasajiliwa leo, hana msaada tena na si faida yoyote kwa klabu na timu, ni jambo baya sana.

 

Tukubali kwamba Yanga inaingia hasara kulipa deni hili kwa mwendo unaojitokeza sasa na mwisho inakwenda kuingia hasara ni klabu maana baada ya hapo yatafuatia madeni na kadhalika.

 

Hasara ya Klabu ya Yanga inabebwa na nani, hasa zile za uendeshaji kesi na zile ambazo zitaongezeka kutoka katika kile ambacho Tambwe anadai.Achana na kujisifi a mitandaoni kwamba sisi tutalipa haina shida, unajua zinatoka wapi?

 

Klabu ni zake au inakopeshwa? Ikiwa hivyo italipaje, kuna riba au kawaida na kama ipo, kiasi gani?Huwezi ukawa na viongozi wanakubali fedha za klabu zitumike kwa uzembe wao. Lazima kuwe na utaratibu ambao unawabana viongozi wazembe wanaoiingiza klabu katika hasara kutokana na uzembe wao.

 

Uongozi lazima urithi wa mali, madeni na mambo mengine. Hivyo kuanza kuleta propaganda katika mambo yanayoonyesha kuna uzembe ikifi kie mwisho na mheshimu mali za klabu kwa kuwa nyie ni watumishi.

MAKALA NA SALEH ALLY

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply