The House of Favourite Newspapers

MSUKUMA ASHAURI TUME IUNDWE KUFELI MIRADI YA MAJI (Video)

MBUNGE wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’  amemshauri Waziri wa Maji, Isaac Kamwelwe aunde tume ambayo itafanya uchunguzi kwa nini miradi mingi ya maji nchini haifanikiwi kama ilivyopangwa.

Msukuma aliyasema hayo leo bungeni akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, ambapo alisisitiza kwamba iwapo waziri hawezi kuunda tume hiyo, basi aliachie bunge liiunde.

Aliongeza kwamba tatizo kubwa linatokana na makandarasi wa miradi ya maji kutopatiwa fedha kwa wakati muafaka, matokeo yake wananchi ndiyo wanaoteseka kwa kukosa maji.

Comments are closed.