The House of Favourite Newspapers

Mtoto Mwingine Mwenye Maajabu Atikisa, Anatibu kwa Maji na Duaa – Video

0

Wakati gumzo la mtoto Eunice Atieno mwenye umri wa miaka miwili na nusu, mkazi wa Kijiji cha Bukama, Rorya mkoani Mara mwenye uwezo wa ajabu wa kutibu kwa kutumia maombi na maji likiwa halijapoa, mtoto mwingine mwenye uwezo wa ajabu ameibuka jijini Dar es Salaam na kuwa gumzo kubwa.

 

Mtoto huyu, anaitwa Sharfat Ally Amini, ana umri wa miaka mitatu na anaishi na wazazi wake, Majohe, Gongolamboto jijini Dar es Salaam.

 

Kwa mujibu wa maelezo ya wazazi wake, Sharfat alianza kuonesha uwezo wa ajabu wa kuponya, akiwa na umri wa mwaka mmoja pekee ambapo alifanikiwa kumponya bibi yake aliyekuwa anaumwa kichwa, kwa kumgusa sikio lake.

 

Kingine kinachoshangaza, ni kwamba licha ya umri wake mdogo, mtoto huyu anaweza kutamka vizuri maneno yaliyomo katika Quran tukufu pamoja na kuhifadhi aya za Quran katika kichwa chake.

 

Wazazi wake wanaeleza kwamba ameonesha uwezo wa ajabu wa kuwasomea watu dua na kuwaponya magonjwa mbalimbali, anaweza kushika vitu vya moto bila kuungua lakini pia, anaweza kuanguka umbali mrefu lakini asisikie maumivu.

Unaweza Kutazama Mahojiano ya Mtoto Huyo kwa Kuingia Global TV Online Hapa

Leave A Reply