The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Mayweather Matatani kwa Kuchoma Mtu Kisu

0
TAARIFA kutokea pande za Marekani ambapo vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuhusu taarifa ya mtoto wa kike wa bondia maarufu duniani Floyd Mayweather aitwae Yaya Mayweather kumchoma kisu Ex wa mpenzi wake.
Inaelezwa timbwili hilo lilitokea Aprili, mwaka 2020 ambapo Yaya alifika nyumbani kwa mpenzi wake, Rapa NBA Youngboy  kisha kumkuta baby wake ambae ni EX wa NBA Youngboy aitwae Lapattra Lashai na kuingia kwenye ugomvi mkubwa wa maneno uliosababisha kugombana kwa wadada hao na Yaya kumchoma kisu mwenzake.
Inaelezwa wivu wa mapenzi umemponza binti Yaya Mayweather ambae taarifa zinasema kwamba huenda akafungwa hadi miaka 20 gerezani kwa kosa hilo la kumchoma kisu Lapattra. Hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kusomwa Februari 2022.
Leave A Reply