The House of Favourite Newspapers

MTOTO WA MIAKA 10 AJITAHIRI KWA KISU

0

Mvulana wa miaka 10 mkazi wa kijiji cha Itare nchini Kenya amejitahiri kwa kutumia kisu  baada ya wazazi wake kushindwa kulipia gharama ya Ksh 1000/- ya kupewa huduma hiyo hospitali. Mtoto huyo wa darasa la pili ameeleza chombo cha habari kimoja nchini humo kuwa alilazimika kufanya hivyo kwa kuhofia unyanyapaa atakaofanyiwa na wenzake ambao wao walifanyiwa toraha kipindi cha likizo ya mwezi Desemba.

Inaelezwa kuwa hali ya mtoto huyo kiafya sio nzuri tangu alipojifanyia kitendo hicho mwezi mmoja uliopita na awali alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kisii lakini wazazi wake walimrudisha nyumbani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Mwanaharakati wilayani Kisii, Samwel Momanyi ameomba serikali iingilie kati na kumsaidia mtoto huyo kupata matibabu kwani anapata maumivu makali sana hususani akijisaidia haja ndogo. Mvulana huyo ameshindwa kuanza masomo le0 Jumatatu baada ya shule kufunguliwa, kutokana na afya yake kutoimarika.

Leave A Reply