The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Miaka 8 Apewa Mimba

0

KATIKA  hali isiyo ya kawaida na kushangaza kiasi cha kusababisha sintofahamu ya kitabibu, mwanafunzi mwenye umri wa miaka minane anayesoma darasa la pili katika shule mojawapo ya msingi wilayani Missenyi mkoani Kagera amepewa mimba!

 

Unashangaa? Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Missenyi, Beatrice Sanga amesema kuna kesi nane za mimba katika shule za msingi mojawapo ndani ya Wilaya ya Missenyi. Wanawapima watoto ujauzito kila baada ya miezi mitatu.

 

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Missenyi, Lucy Eustace anasema mtoto wa kike mwenye umri wa miaka nane anaweza kubeba mimba endapo yai litakuwa limekomaa na mji wa uzazi umejiandaa kwa ajili ya kupokea mtoto kama atakutana na mwanaume.

 

Anasema taarifa za hospitali zimethibitisha mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) ni mjamzito.

“Najua inashangaza wengi, lakini lazima mtambue kuwa ni mara chache mtoto wa miaka minane kubeba ujauzito ingawa mtoto anaweza kupata mimba kama yai limekomaa na mji wa mimba umejiandaa kupokea mtoto,” anasema Eustace.

 

Leave A Reply