The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Shah Rukh Khan Atoka Gerezani

0

Mtoto wa muigizaji maarufu kutoka India, Shah Rukh Khan ametoka gerezani kufuatia kesi iliyokuwa inamkabili ya kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya nchini humo.   

                            

Aryan Khan mwenye miaka 23 alikamatwa na polisi tangu Oktoba 3 mwaka huu na wenzake, huku akiwa  amekaa gerezani kwa muda wa siku 26 tangu kukamatwa kwake.

 

Jana Jumamosi, mahakama ya nchini India imemuachia kwa dhamana Aryan Khan huku mashabiki na wapenzi wa filamu za baba yake Shah Rukh Khan wakimpokea kwa furaha na ndelemo mtoto huyo wa staa wa filamu India.

 

Mamlaka ya kudhibiti madawa ya kulevya nchini India ilisema Khan anahusika na biashara ya kuuza madawa ya kulevya baada ya kukuta mawasiliano katika simu yake na wasafirishaji wa madawa ya kulevya kupitia mtandao wa WhatsApp.

 

Lakini mwanasheria wa Khan ameeleza mahakama kuwa Aryan Khan hakukutwa na aina yoyote ya madawa ya kulevya na suala la kuwa na mawasiliano na wasafirishaji wa madawa ya kulevya halina ukweli wowote.

Cc; @bakarimahundu

Leave A Reply