The House of Favourite Newspapers

Muhimbili Yamsaka Aliyevujisha Video ya Prof. Jay ICU

0

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imesema inashirikiana na mamlaka nyingine kumpata mtu aliyemrekodi video Prof. Jay, ambaye anapatiwa matibabu hospitalini hapo.

Video hiyo iliyosambazwa mitandaoni inamuonesha msanii huyo akiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum.

Hospitali hiyo imesema kwamba video husika haikurekodiwa na kusambazwa na hospitali, na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na imani nayo pamoja na kuheshimu taratibu za hospitali.

Leave A Reply