The House of Favourite Newspapers

Mujini shule, jiongeze!

0

Je, wewe ndiyo unaingia mjini? Kama ni hivyo kwa kweli naona nichukue muda huu kutoa semina fupi kwako kuhusu mambo ya MUJINI. Kimsingi sentensi isemayo ‘Mjini Shule’ ni ya kweli kabisa na ni muhimu kuiweka kichwani mara tu utakapoingia  mjini, kwa taarifa mjini ni kuanzia Chalinze.

Somo la leo nitaanza kwa kukuonyesha sentensi ambazo kwa asilimia karibu mia moja ni za uwongo, usiziamini kabisa, ila umeingia mjini utazisikia sana. Kaa chonjo!

Sentensi ya kwanza utakayoisikia kutoka kwa mupenzi wa kimujini, ukisikia mdada anakwambia ‘Ki ukweli siko peke yangu, nina boifrend wangu yuko nje ya nchi anasoma’……hii ni sentensi ya kukufanya usimuulize inakuwaje ana maisha mazuri wakati hana kazi na anaishi peke yake.

Hapa unawekwa sawa na muda si mrefu na wewe utageuka kitega uchumi kingine, hapa mjini utaitwa BUZI au ATM au SERIKALI na ukiwa fala sana utaitwa pedeshee. Sentensi nyingine kali utakayosikia hapa mjini ni  ‘Sijichubui weupe huu umekuja kwa sababu ya maji ya Dar es Salaam’…..hahahahahahaha hapa nacheka tu, utakuwa fala kuamini mke uliemuoa mweusi anabadilika rangi kwa ajili ya maji ya bomba, ila wako wenzio wengi wanaamini rungu hili!

Siku ukisikia mpenzi anakuambia ‘Nilienda Arusha kuna kaka’ke rafiki yangu kanikopesha milioni 3 za kuanzia biashara. Lakini hakunidai chochote’………….jiulize wewe huyo mdada ungeweza kumpa milioni 3 halafu kisitokee chochote? Mwisho ukisikia sentensi hizi ‘Sikupendi kwa ajili ya hela yako, I love you for who you are’!

Hizi sentensi hutumika pia na wanasiasa ambao hudai hawataki ubunge kwa ajili ya kipato bali wanataka kusaidia wananchi, teh teh teh chezea mkwanja wewe, sasa kama utaiamini shauri zako, mjini shule. Ukiwa na mupenzi akaanza kukwambia ‘Yule ni rafiki yangu wa kawaida tu’ Ndugu yangu unaeingia mjini, hakuna kitu kama hicho hapa mjini, hapo ujue kuna jipu.

Ukisikia umejibiwa ‘I love u too’, ina maana umeanza wewe kwa kujiona mjanja na kusema ‘I love you’, na hii ni hatari kwani ina maana umeshapoteza uwezo wako wa kuwaza sawasawa. Akili imeshasiz!

Leave A Reply