The House of Favourite Newspapers

Mumeo Anachepuka, Hampati Watoto? Tazama Hii – Video

0

WATU wengi wamekuwa wakitamani mafanikio ya watu Matajiri pasipo kufahamu changamoto za kimaisha zilizowainua kwenye maisha yao mpaka kufanikiwa kwao kwa kutofikiri namna ya kujifunza kupitia hizo changamoto ili nao wainuke kimaisha.

 

Dkt. Getrude Rwakatare ambaye ni Mchungaji Kiongozi wa Makanisa ya Mlima wa Moto, Mmiliki wa Shule za St Mary’s International na Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya CCM, kupitia mahojiano haya amezungumzia mambo mengi kuhusu ndoa, maisha ya wanandoa na kugusia Maisha yake kwa ufupi ili kuwafungua watu wengi ambao wanadhani ndoa ni suala la mchezo.

 

Mbali na hivyo amezungumzia Kongamano la wanandoa analolifanya kila mwaka la Mariage Revival Dinner Party juu ya umuhimu wa Kongamano hilo na jinsi litakavyofana mwaka huu ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam, Machi 6, 2020. Pia, siku ya Wanawake itakayofanyika Diamond Jubilee hall Machi  8, 2020.

 

Leave A Reply