The House of Favourite Newspapers

Muna Love: Namkataa Shetani

0

MSANII wa Bongo Movies, Rose Alphonce Nungu maarufu kama Muna Love baada ya kuwaasa Watanzania kutofanya sajari za kubadilisha maumbo yao, leo amekuja na hili.

“Bwana Yesu. 🙌🏻🙌🏻🙏🏼 Ahsante kwa kunipenda, Ninakushukuru kwa kufa msalaban kwa ajili yangu mimi, nakuja mbele zako nina jua mimi ni mwenye dhambi Naomba unisamehe dhambi zangu zote.

Ninajua kwa kukutenda dhambi Jina langu liliingia kwenye kitabu cha hukumu. Nimesimama leo Yesu Naomba unisamehe ,unifute Jina langu kutoka kwenye kitabu cha hukumu , nauliandike kwa upya kwenye kitabu cha uzima.

Nina kukaribisha karibu ndani yangu uwe bwana na mwokozi kuanzia leo uniongoze , unifundishe unielekeze njia ya kuendea katika Maisha yangu kipindi hiki cha msimu Mpya karibu ndani yangu.

Nina mkataa SHETANI peupe kabisa na kazi zake zote, na uongo wake wote, ninakupokea wewe Yesu WANGU, Bwana Yesu ulipoondoka uliniahidi hutaniacha.

utanipa msaidizi atakaa na mimi. Na mimi leo kwa kukukiri wewe YESU ninamuomba msaidizi aje ndani yangu anijaze nguvu niweze kuishi maisha ya ushindi niweze kuishi maisha ya kukutumikia wewe.

niweze kukaa katika zamu yangu ya maombi kipindi hiki cha uamsho na msimu mpya. Roho mtakatifu ninakuhitaji karibu ndani yangu unijaze nguvu.

Nguvu za kushinda, nguvu za kushuhudia, nguvu za kusonga mbele, nguvu za kuondoa uchovu na magonjwa, nguvu za kusimama kwenye kusudi uliloniitia 🙏🏼”.

Leave A Reply