The House of Favourite Newspapers

Muna Yuko Hoi Kisa Sajari?

0

IMEDAIWA kwamba, kwa wiki ya pili sasa, msanii wa Bongo Movies, Rose Alphonce Nungu haonekani huku tetesi zikisema kuwa sajari zimedunda hivyo yupo mahututi.

Hata hivyo mwenyewe ameibuka na kudai kwamba anaoeneza habari hizo ni watu wasiomtakia mema na kwamba wanamchuria kwani hana hata homa.

“Mimi nipo salama kabisa sina chochote kinachonisumbua hata homa sina kwa kifupi sipo mahututi, ila hao wananichuria na kuniombea mabaya waache maana Mungu anayenilinda ataniepusha na mabaya yote wanayonisingizia, sina shida shida kabisa na naendelea kupendeza kwa jina la Yesu maana ndiye aliyenipa maarifa yote,” anasema Muna.

Taarifa ikufikie kwamba, Muna amefanya upasuaji au sajari za kutengeneza Dimpoz kwenye mashavu yake kisha akafanya sajari ya kurekebisha midomo na nyingine; jumla yake ni kumi na moja.

Leave A Reply