The House of Favourite Newspapers

Muonekano wa Uwoya Washtua

0

MUONEKANO wa msanii wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya kwenye picha inayosambaa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, umewashtua wengi kwani inamuonyesha akiwa mwenye umbo tofauti na picha zote ambazo hutupia kila siku.

 

Picha hiyo ilisambaa kwenye kurasa kibao za wambea huku Instagram na watu kuanza kushusha maswali yao kwamba umbo zuri ambalo amekuwa akionekana nalo kwenye picha zake anazotupia analitoaga wapi kama siyo kuji-editi.

 

“Duh, kweli duniani kuna mambo, sasa lile umbo analojinadi nalo kwenye mapicha yake ya kila siku kumbe ni feki anaji-editi, hawa mastaa wana shida maana angalia sasa ameumbuka kwani akijiposti kama alivyo kuna tatizo gani kuliko kudanganya watu,” yalisomeka baadhi ya maoni ya wafuasi hao.

 

Leave A Reply