Musukuma Akumbuka Kikwete Alivyomuibua Kisiasa

MBUNGE wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma, amesema kwamba maneno ‘Utakumbukwa Kikwete’ yaliyobandikwa kwenye baadhi ya mabasi yake ni ishara ya yeye kumuenzi kiongozi huyo mstaafu ambaye alimwinua kisiasa na kufikia ngazi aliyopo sasa.

Joseph Kasheku Musukuma.

Akifafanua zaidi alisema ujumbe huo unakumbusha pia mambo ya maendeleo aliyoyaanzisha kwa Watanzania na ambayo yanaendelezwa na utawala wa awamu ya tano sasa.

“Kikwete alinisaidia kuingia kwenye siasa; nimeingia katika siasa wakati wa Kikwete.  Kwa hiyo nikisema tutamkumbuka ninamaanisha tutaendelea kumkumbuka kwa mema yote aliyotufanyia.”

Aidha aliongeza kwamba si basi moja tu lililoandikwa maneno hayo,  kwani yapo mengine tisa  yenye ujumbe huo.

Salum Milongo/GPL


Loading...

Toa comment