The House of Favourite Newspapers

Mwakyembe: Rais Mpya TFF Ataapishwa Leo

0
Waziri wa Habri, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu waTFF, Dodoma.

TOFAUTI na miaka iliyopita ya rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuapishwa siku chache baada ya uchaguzi lakini leo hapa Dodoma ambapo unafanyika uchaguzi, rais ataapishwa muda mfupi baada ya kushinda.

 

Mwakyembe akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi wa TFF.

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika leo mjini hapa kwenye Ukumbi wa St Gasper kwa ajili ya kuwapata washindi wa nafasi ya urais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.

 

Mwakyembe akizungumza na Mtangazaji wa Azam TV, Charles Hilary.

Uchaguzi huo unasimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli unafanyika baada ya Jamal Malinzi kuelekea kumaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka minne.

Mwakyembe akibadilisha mawazo na viongozi wa TFF.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr, Harrison Mwakyembe amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu na waandishi wa habari.

Nje ya Ukumbi.

Mwakyembe amesema rais na wajumbe watakaopatikana leo wataapishwa mbele ya wapiga kura wote wa uchaguzi tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakishahau haki ya waliowachagua kwa kuwaapisha nje ya utaratibu.

Mgombea Urais wa TFF, Imani Madega akiwasili eneo la uchaguzi.

 

Musa Mateja | Global Publishers |Dodoma

 

Leave A Reply