The House of Favourite Newspapers

MWALIMU AKAMATWA KWA KUZINI NA KIVULANA

 

Stephanie Peterson anayedaiwa kumghilibu mwanafunzi wake wa miaka 14 wa kiume na kuzini naye.
Picha ya Peterson akiwa mikononi mwa polisi ambapo ilifahamika pia kwamba alikuwa anamnunulia mtoto huyo bangi na kumfundisha jinsi ya kuivuta.
Peterson akiwa na mumewe, Brandon, ambaye wameoana tangu 2015.

 

STEPHANIE PETERSON (26) mwalimu wa kike wa shule ya msingi huko New Syma, Florida, Marekani,  amekamatwa wiki hii kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na  mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14.

 

Mwalimu huyo alianzisha uhusiano huo na kivulana hicho mwezi Novemba mwaka jana kwa kukitumia picha za watu walio uchi.  Isitoshe, kwa mujibu wa polisi, mtoto huyo amesema mwalimu huyo alikuwa anamnunulia bangi na kumfundisha jinsi ya kuitumia.

 

Kutokana na kashfa hiyo ya kuonyesha tabia za kiasherati, Peterson ambaye ni mke wa Brandon tangu mwaka 2015 walipooana, tayari amejiuzulu nafasi yake katika shule hiyo alikokuwa mwalimu wa sayansi.  Mwalimu huyo na mumewe bado hawajapata mtoto.

 

Peterson ambaye yuko nje kwa dhamana ya Dola 25,000, alimwambia mtoto huyo asimwambie mtu yeyote juu ya uhusiano wao huo.

 

Mtoto huyohuyo ndiye aliyefichua juu ya uhusiano wake huo na mwalimu ambapo anasemekana kuwaambia pia wazazi wake kwamba uhusiano huo ulifanya uwezo wake darasani upungue

 

Vilevile alisema Peterson ambaye jina lake la ndoa ni Ferri, kila mara alikuwa akimchukua nyumbani kwao saa tano za usiku na kwenda naye sehemu za siri.

 

WALUSANGA NDAKI/ MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI

 

Comments are closed.