The House of Favourite Newspapers

MWANA FA: MIE HISPANIA ILA BRAZIL MABINGWA

Kikosi cha imu ya Taifa ya Hispania

STAA wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki wa timu ya Taifa ya Hispania, lakini anaona wazi kuwa Brazil ndiyo watakuwa mabingwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko Urusi.

 

Mwana FA licha ya kuwa msanii pia amekuwa akifuatilia kwa ukaribu mkubwa ligi mbalimbali za soka na sasa michuano ya Kombe la Dunia, ameonekana kuzikandia timu pinzani kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii huyo alisema: “Timu zenye nafasi ya kutinga nusu fainali hadi fainali ni Ufaransa, Ureno, Hispania na Brazil, lakini kati ya hizo zote, timu ambayo imekamilika kila idara yaani kuanzia kwa kipa hadi wachezaji wa ziada ni Brazil, wana nafasi ya kuwa mabingwa.

 

“Mimi ni shabiki mkubwa wa kikosi cha Hispania, kimekamilika kutokana na wachezaji wake wengi kucheza ligi moja (La Liga ya Hispania), hivyo ukiangalia kwa haraka utaona kama wamezoeana ingawa ukweli utabaki kuwa kikosi changu hicho hakiwezi kuwafikia Brazil ambao wao wamekamilika zaidi.

Comments are closed.