The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Asimulia Alivyobakwa na Kupata Ujauzito

0

MWANAFUNZI wa kidato cha nne ambaye pia ni shahidi wa kwanza kwenye kesi ya ubakaji inayomkabili Boniface Malila (20), amedai kumtambua mshtakiwa huyo kuwa ndiye aliyempatia ujauzito.

 

Mshtakiwa huyo, mkazi wa kijiji cha Katemwa, Chato mkoani Geita, anakabiliwa na kesi ya kumbaka na kumsababishia mimba mwanafunzi huyo wa kidato cha nne (jina lake na shule vinahifadhiwa).

 

Mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Chato, mwanafunzi huyo ambaye aliongozwa na mwendesha mashitaka wa polisi, Mauzi Lyawatwa, alisema jana kuwa anamtambua mshtakiwa (aliyekuwa kizimbani) kwamba ndiye aliyempatia ujauzito baada ya kufanya naye mapenzi kwa nguvu kwenye nyumba ya kulala wageni ya “Double M” iliyoko Katemwa.

 

Alidai kuwa alishawishiwa na rafiki yake (jina linahifadhiwa) ambaye pia ni mwanafunzi mwenzake kuwa waongozane kwenda Muganza kumsalimia shangazi yake pasipo kujua kama ilikuwa njama ya kumkutanisha na mshtakiwa.

Leave A Reply