The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Mwenye Matatizo ya Akili Aambukizwa Ukimwi- Video

0

Fatuma Athumani (60) ni mama ambaye alibahatika kupata watoto Tisa, lakini watoto wawili kati yayo walifariki dunia huku mmoja akifariki kwa kujinyonga kutokana na kutokuelewa na baba yake mzazi.

 

 

Watoto watatu kati ya watoto 9 kwa sasa wanaugua ugonjwa wa akili ambapo wakike ni wawili na wakiume mmoja na watoto hao wote walibahatika kusoma huku chanzo cha kuugua ugonjwa huo kinasikitiaha kwani kila mmoja ulimuanza katika hali tofauti.

 

 

Akisimulia kwa uchungu mama huyo anasema ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote wamemtenga kutokana na matatizo anayoyapitia kutokana na watoto wake hao.

 

 

Kwasasa hali ya baba mzazi wa watoto hao ni mbaya zaidi kwani hana uwezo wa kufanya chochote kile zaidi ya kulala kutokana na matatizo ya Presha na Kisukari. Mama huyu anahitaji msaada wa mtaji wa biashara ya mkaa ambayo alikuwa akiifanya hapo awali pamoja na vyakula.

 

0657 306 264 – Fatuma Athumani

 

 

Leave A Reply