The House of Favourite Newspapers

Mwanaume Afunga Ndoa na Rice Cooker

0

MWANAUME mmoja nchini Indonesia, Khoirul Anam amefunga ndoa na Rice Cooker ili liwe ndo mke wake.
Ndoa hiyo imefungwa tarehe 20 septemba 2021 ambapo bwana harusi alivaa mavazi rasmi kwa ajili ya harusi hiyo na kupewa cheti cha ndoa kwa kuoa chombo hicho cha umeme cha kupikia wali.

Rice Cooker hiyo ilivalishwa mtandio katika siku hiyo muhimu ya kwenda kuanza maisha mapya ya ndoa.
Khoirul Anam anasema kuwa yeye ni mweupe(fair) na hapendi kuzungumza sana na pia anapenda kupika na amelipenda sana Rice cooker hilo na kuamua kulioa kabisa liwe mke wake huku akilimwagilia mabusu ya Upendo.

Baada ya ndoa hiyo iliyo waacha watu midomo wazi jamaa huyo alipost picha mitandaoni za siku yake hiyo ya muhimu ya kufunga ndoa ingawa bado hajapost picha zao za fungate(Honey moon) na mkewe huyo.

Leave A Reply