The House of Favourite Newspapers

Mwasiti: Sipendi Mwanaume Mchafu!

0

MAMBO vipi msomaji wa safu yako pendwa ya My Style? Kama ilivyo kawaida, hapa tunakutana na mastaa mbalimbali nchini na kupiga nao stori mbalimbali kuhusu life style yao mbali na kazi wanazofanya.

Leo tupo na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almas, ambaye ametamba na nyimbo kibao ikiwemo Nalivua Pendo na nyingine nyingi.

Amefunguka mambo mengi usiyoyajua, ungana nami kwa mahojiano zaidi:

My Style: Ratiba yako kwa siku ikoje?

Mwasiti: Unajua mimi ni Muislam, kwa hiyo mara nyingi nikiamka tu asubuhi, kitu cha kwanza naswali, nikishamaliza nakimbia kidogo kisha nikirudi ndio nakunywa maji glasi mbili na baada ya hapo kwa kuwa napenda sana kuandika, hivyo nachukua kompyuta na kuanza kuandika kitu chochote ambacho nitajisikia kuandika siku hiyo.

My Style: Sehemu gani ya starehe ambayo huwa unapenda sana kwenda?

Mwasiti: Napenda kuangalia muvi, kuangalia mpira na mara nyingi naangalia nyumbani kwangu au nikiwa nimepata mwaliko kwa rafiki yangu kwa sababu mimi ni shabiki sana wa mpira na kwenda kuangalia uwanjani, labda iwe inacheza Simba na Yanga.

My Style: Unapokuwa na msongo wa mawazo, unapenda kufanya nini ili uwe sawa?

Mwasiti: Nacheza Basketball, hivyo ninavyokuwa kichwa kizito naenda uwanjani kucheza. Hapo ndipo nitakuwa sawa narudi nyumbani mwepesi.

My Style: Unapendelea chakula na kinywaji gani?

Mwasiti: Napenda sana ugali samaki na tembele, kinywaji ni soda.

My Style: Unapenda kutoka ukiwa katika muonekano gani?

Mwasiti: Napenda kutoka nikiwa simple lakini niwe safi nimependeza.

My Style: Unapokuwa nyumbani, ni kitu gani unapendelea kufanya?

Mwasiti: Napenda sana usafi, mimi sipendelei kuona uchafu kabisa, muda mwingi utanikuta nasafisha nyumba.

My Style: Unapenda mwanaume mwenye sifa zipi?

Mwasiti: Awe mcha-Mungu inatosha, hela baadaye.

My Style: Unapotoka na mpenzi wako, unapendelea awe katika muonekano gani?

Mwasiti: Sipendi mtu mwenye makuu. Napenda awe gentle men, avae simple kama ni shati, suruali kawaida tu lakini apendeze.

My Style: Ni mwanaume wa aina gani akikufuata huwezi kukubali hata kwa chochote?

Mwasiti: Mwanaume mchafu asiyejielewa, hapo siwezi kukubali. Kabla ya kuwa katika uhusiano, nilikuwa naangalia sana hicho kitu.

My Style: Mavazi yako unabuni mwenyewe au kuna mtu?

Mwasiti: Inategemea na tukio lenyewe, ndipo atakuwepo mtu wa kunibunia, katika mambo yangu ya kawaida nabuni mwenyewe.

My Style: Unapenda mtoto wa kwanza awe jinsia gani?

Mwasiti: Yeyote, siwezi kumpangia Mungu maana mtoto ni mtoto tu.

My Style: Tangu tumeanza kukujua, unaonekana kuwa na ngozi nzuri, je huwazi kujichubua?

Mwasiti: Napaka Bio Oil na siwazi hata siku moja kujichubua, napenda ngozi yangu ilivyo.

My style: Ni msanii gani hapa Bongo anakuvutia na mavazi yake?

Mwasiti: Ni wengi wanavaa vizuri maana kila mtu ana aina yake ya mavazi, hivyo mtu akivaa akapendeza mimi napenda.

My Style: Wewe ni chizi nini?

Mwasiti: Mimi ni chizi viatu sana tu.

My Style: Una pair ngapi na kiatu chako cha gharama ni kipi?

Mwasiti: Nina pair nyingi sana, sijawahi kuhesabu, nanunua gharama yoyote inaweza ikawa hata laki mbili kama nimekipenda na kiwe kiatu imara.

My Style: Unapendelea rangi gani za nguo ambazo zinakuvutia?

Mwasiti: Napenda rangi za dunia kama nyeusi na nyeupe maana ni rangi ambazo unaweza ukavaa na kitu chochote na ukapendeza.

My Style: Ni aina gani ya nguo ukivaa unakuwa comfortable?

Mwasiti: Nikivaa gauni ya mikono mirefu alafu likiwa fupi na simple raba, jeans na tshirt nakuwa comfortable na ninapenda.

My Style: Katika handbag yako, ni kitu gani hakikosekani?

Mwasiti: Haikosekani leseni ya udereva, picha ya mama yangu, card za bank na haikosekani pesa hata kidogo angalau niwe na laki ya dharura.

My Style: Ni kitu gani unakichukia katika mitandao ya kijamii?

Mwasiti: Sipendi watu ambao wanao-comment hovyo katika mitandao bila hata kuangalia kitu wanacho-comment, nachukia sana na nimejifunza siwezi kumjibu mtu mpaka niangalie profile yake nimjue ni mtu wa aina gani.

My Style: Kuna baadhi ya wasanii wamekuwa na sifa kubwa ya kudanga ili wapate pesa ya kujikimu, kwa upande wako unawashauri nini?

Mwasiti: Inabidi wajitathimini sana maana kuna wakati unafika hivyo vitu vinagota, inabidi ufanye maisha yako tu.

My Style: Neno la mwisho kwa mashabiki wako.

Mwasiti: Nawapenda sana!

My Style: Unapendelea chakula na kinywaji gani?

Mwasiti: Napenda sana ugali samaki na tembele, kinywaji ni soda.

Leave A Reply