The House of Favourite Newspapers

Mwigulu: Nyalandu Alinyoosha Suti Zake Ulaya, Lissu Amelipwa

0

MGOMBEA ubunge Iramba Mashariki Mkoa wa Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mwigulu Nchemba, ameanza kumchokonoa Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Lazaro Nyalandu, mgombea ubunge wa Singida Kaskazini.

 

Akizungumza kwenye kampeni za Dk. John Magufuli,  ambaye ni mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM katika Uwanja wa Bombadier mkoani Singida, Septemba 1, 2020, amesema, wawili hao hawana uzalendo.

 

Bila kuwataja majina, Mwigulu alimnanga Nyalandu kwamba, alipokuwa waziri (Waziri wa Maliasili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne) alikuwa akienda Ulaya kunyoosha suti zake huku Lissu akisema amerejea nchini baada ya kupewa ‘advance’ (malipo ya awali).

 

Lissu alirejea nchini akitokea kwenye matibabu nchini Ubelgiji.  Ni baada ya watu wasiojulikana kumshambulia kwa risasi ‘Area D,’ jijini Dodoma Septemba 7, 2017.

 

Mara kadhaa Lissu alinukuliwa na vyombo vya habari akiwa ughaibuni, kwamba alishindwa kurudi Tanzania kwa kuwa si sehemu salama kwake.

 

“Wengine wanakuja hapa wanajifanya watoto wa Singida, hawana uzalendo hata na wana-Singida. Kuna mmoja tulikuwa mawaziri wote, hata suti zake alikuwa anaenda kunyoosha Ulaya, hana uchungu na Singida.

 

“Mwingine alisema Tanzania si salama, sasa hivi amekuja sababu ‘advance’,  amechukua baada ya uchaguzi tu atasema, Tanzania haiko salama, ataondoka,” amesema Dkt. Mwigulu.

 

Mwigulu ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria, amewataka Watanzania kumchagua Rais Magufuli. “Ioneeni huruma Tanzania, wale wagombea wengine wote mimi nawafahamu na nikiangalia janjajanja yao, naona hata ‘advance’ wamechukua, nchi yetu itauzwa mkimuacha Dk. Magufuli,” amesema  Mwigulu.

 

Leave A Reply