The House of Favourite Newspapers

MWILI WA MVUMBUZI WA TANZANITE WAAGWA DAR, WAPELEKWA SAME KUZIKWA

Mtoto wa marehemu huyo, Hassan Ngoma (kulia) akizungumza na wanahabari baada ya kumswalia marehemu.

 

MWILI wa Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, mzee Jumanne Ngoma (84) aliyefariki dunia juzi Jumatano, Januari 30, 2019, umeaswaliwa katika msikiti wa Masjid Maamur, Upanga jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Makanya, Same mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.

 

Hassan Ngoma akiwa na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) baada ya kuuswalia mwili wa marehemu.

 

Mzee Ngoma alifariki katika Hospitali ya Taifa Hospitali Muhimbili (MNH) alipokuwa amelazwa akitibiwa.

Baada ya mwili huo kuswaliwa msikitini hapo waombolezaji walirudi tena Muhimbili kwa ajili ya safari ya kuelekea Makanya kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho kijijini hapo.

 

Huu ndiyo msikiti alioswaliwa marehemu. HABARI: ZAINA MALOGO
PICHA: RICHARD BUKOS

Mwili wa Aliyegundua Tanzanite Ukiswaliwa Msikitini

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.