The House of Favourite Newspapers

Mzee Mpili: Mechi ya Kigoma Imekwisha

0

SHABIKI na mwanachama maarufu wa Klabu ya Yanga mzee Haji Mpili ameweka wazi kuwa ushindiwa bao 1-0, walioupata dhidi ya Simba, Julai 3, 2021 yeye ndio alicheza mchezo huo na kuhakikisha Simba haishindi.

 

Mzee Mpili ambaye alionekana na badhi ya viongozi wa juu wa Yanga siku kadhaa kabla ya mechi amesema alichokifanya kwa Mkapa ni siri yake na atakifanya tena kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Azam Shirikisho kati ya Yanga na Simba, itakayochezwa katika Dimba la Tanganyika mjini Kigoma, Julai 25, 2021.

 

“Hii ya tarehe 3 ilikuwa salamu tu derby yenyewe ni tarehe 25 Kigoma kwa sababu Simba wana kelele sana na kelele zao tunajua akina nani wanawaoa hizo kelele, mimi ndo nilikuwa mchezaji namba moja wa ule mpira na Kigoma ndo utachezwa mpira wa uhakika” amesema Mzee Mpili.

 

“Mchezo wa Kigoma nimeshamaliza kazi, Kigoma hawatoki ng’ooo, niache kama nilivyo hawatoki. Wapeni habari kwamba Mzee Mpili amesema kama alivyowamenyeni Dar es Salaam na Kigoma mtawamenywa, tena magoli ya Kigoma ni ya kuhesabu.

 

“”Mechi ya juzi nilijua tutashinda, hata kama Simba angetangulia kufunga ningesawazisha na kuongeza goli la pili. Tunajua Simba inajipanga kulipa kisasi kwenye mchezo wa Fainali ya FA lakini tayari wamechelewa Kigoma wanakufa tena na shughuli imeisha, tunawapiga tena.

 

“Nimepewa guarantee asilimia 100 kuwa Mechi ya Kigoma imeisha na tutashinda goli mbili kwenda mbele . Kama Wanasema jumamosi tulibahatisha sawa, Lakini Shughuli yote wataiona kigoma, hatuwezi kuliacha hilo Kombe,” amesema Mzee Mpili ambaye kwa sasa ana-trendi mitandaoni kila kukicha.

 

Yanga inasubiri kukutana na Simba kwa mara ya ne kabla ya kukamilisha msimu huu huku ukiweka rekodi ya kutokufungwa na Simba kwenye michezo mitatu mfululizo.

Leave A Reply