The House of Favourite Newspapers

Mzee Yusuf Gari Limewaka

0

GARI limewaka! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia moto wa burudani anaoendelea kuuwasha Mfalme wa Taarab Bongo, Mzee Yusuf ambaye amezidi kuthibitisha kwamba, hana mpinzani kwenye muziki huo.

 

Kwa mara nyingine, Mfalme Mzee Yusuf amefunika ile mbaya kwenye shoo matata aliyopiga usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar ambapo alikuwa akilizindua upya kundi lake la Jahazi Modern Taarab.

 

Mzee alipiga shoo hiyo kwa mara ya pili ukumbini hapo, baada ya ile ya Narudi Mjini ambayo ilikuwa ya kwanza tangu arudi kwenye ulimwengu wa Taarab. Katika shoo hiyo, Mzee Yusuf alizindua rasmi kundi lake na kulipa jina lilelile la Jahazi Modern Taarab.

 

Kabla ya kuzindua jina hilo, aliwauliza mashabiki kama walikuwa wakipenda alipe jina gani kundi hilo, ambapo umati mkubwa uliokuwa ukumbini hapo, ulilipuka kwa mayowe na kusema; “Jahaziii…”

Huku wachache wakisema; “Safinaaa…” Ule msemo wa wahenga usemao ‘wengi wape’ ndiyo uliochukua nafasi ingawa hata hivyo, jina la Jahazi lilikuwa limeshaandaliwa, hivyo kilichofanyika ni kulizindua tu.

 

Katika kundi hilo, Mzee Yusuf alikuwa na waimbaji wake aliokuwa nao Jahazi la kwanza akiwemo Khadija Yusuf, Miriam Amour, Mishi Zele, Fatma Kassim, Mwasity Mbwana, Ally Jay, Mussa Mipango, Jumanne Ulaya na wengineo ambao bado yupo nao.

 

Baada ya utambulisho wa kundi hilo, ndipo Mzee Yusuf akaangusha shoo ya kihistoria kama kawaida yake, ambapo mashabiki wengi walikubali kwamba, gari sasa limewaka!

 

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilipotaka kupata maoni yake juu ya namna mashabiki walivyompokea baada ya kurudi kwenye gemu, Mzee Yusuf alikuwa na haya ya kusema; “Kwanza nashukuru kwa sapoti yao, wengi wananiambia walikuwa wamenimisi. Ninawaahidi mambo mazuri yanakuja, hivyo waendelee kunisapoti.”

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

Leave A Reply