The House of Favourite Newspapers

Mzee yusuf, Vanessa kuipeleka Mashallah Dar Live

0

Mashalaa---KKKKKMfalme wa Muziki wa Taarab, Mzee Yusuf akiwa na Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

Na Mwandishi Wetu
MFALME wa Muziki wa Taarab, Mzee Yusuf kwa kushirikiana na staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ wanatarajia kuupeleka wimbo wao mpya wa Mashallah Januari 30, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko mratibu wa shoo hiyo, Seif Magwallu ‘Shiboli’ alisema kuwa usiku huo utakuwa maalum kwa uzinduzi wa albamu mpya ya Jahazi iitwayo Kaning’ang’ania.

“Mashabiki watapata kuzisikia kwa mara ya kwanza nyimbo zilizopo katika albamu mpya kama vile Hilo Limekuuma ya Fatma Ally, Nia Safi Hairogwi ya Mish Mohyamed, Nina Moyo Sina Jiwe ya Leila Rashid pamoja na Mashallah ya Mzee Yusuf akiwa na Vanessa Mdee,” alisema Shiboli na kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa shilingi 10,000 tu getini.

Leave A Reply